Campaign: WPWP Tanzania

"Kurasa za Wikipedia Zinazohitaji Picha" (Wikipedia Pages Wanting Photos- WPWP) ni mashindano ya kila mwaka ambapo Wanawikipedia katika miradi ya lugha zote wanaongeza picha kwenye Wikipedia makala zinazokosa picha. Hii inalenga kutumia picha nyingi zilizokusanywa tayari kupitia mashindano mbalimbali za kupiga picha kwenye WP zinazopatikana kwenye kurasa za Commons lakini hadi sasa hazitumiwi kwenye makala za WP. Picha si mapambo tu ya matini iliyoandikwa bali husaidia kuelewa habari za makala vizuri zaidi.

Maelfu ya picha zimeshaandaliwa na kutolewa kwenye Wikipedia Commons kupitia miradi mbalimbali pamoja na mashindano ya kupiga picha ya kimataifa kama vile Wiki Loves Monuments, Wiki Loves Africa, Wiki Loves Earth, Wiki Loves Folklore, nk. Lakini chache za picha hizi zimetumika kwenye makala za Wikipedia. Leo hii akiba ya Wikimedia Commons inatunza mamilioni ya picha lakini sehemu ndogo tu zimetumika kwenye kurasa za makala za Wikipedia. Mradi huu unataka kupunguza pengo hili kubwa.